Ijumaa 30 Januari 2026 - 08:30
Mirza al-Na’ini ana mchango mkubwa na haki kubwa juu ya hawza za kielimu

Hawza/ Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia nchini Afghanistan amesema kuwa; marehemu Ayatullah al-‘Udhmaa Mirza al-Na’ini ana haki kubwa juu ya wanazuoni na hawza za kielimu, na akaeleza kuwa, kuandaliwa kwa kongamano la kimataifa la kumkumbuka fakihi huyu mashuhuri ni hatua inayofaa na ya lazima.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Muhammad Hashim Salehi, Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Afghanistan, katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, alieleza umuhimu wa kuandaliwa kwa kongamano la kimataifa la kumuenzi marehemu Ayatullah al-‘Udhmaa Mirza al-Na’ini, akisema kuwa; hatua hiyo ni ya heshima na inalingana na hadhi ya kielimu ya fakihi huyo mkubwa. Aliongeza kuwa; marehemu al-Na’ini alistahili kufanyiwa kongamano kubwa, lenye uzito wa kielimu na la kiwango cha juu cha hawza.

Huku akisisitiza kuwa Mirza al-Na’ini ana haki kubwa juu ya hawza za kielimu, alisema kwamba; wanazuoni wengi wakubwa walikuwa miongoni mwa wanafunzi wake; akiwataja watu mashuhuri kama marehemu Ayatullah al-‘Udhmaa Abu al-Qasim al-Khu'i na marehemu shahidi Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr, ambao wote walikuwa wanafunzi wa mwalimu huyu mkubwa. Marehemu Mirza al-Na’ini, kwa upande wa fiqhi na elimu ya usul, alikuwa na fadhila kubwa na umahiri wa hali ya juu katika fiqhi na usul.

Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Afghanistan alibainisha kuwa; kumbukumbu kama hii ingeweza kuandaliwa mapema zaidi, akasema: Ingawa hatua hii imechelewa, hata hivyo ni kazi yenye thamani kubwa, na ni lazima harakati hii iendelezwe pia katika siku zijazo.

Aliongeza kuwa; wanazuoni wanapaswa kuthaminiwa na kuenziwa daima, hususan wale ambao katika uhai wao waliwatumikia watu, Uislamu na hawza za kielimu, na wakawalea wanazuoni wakubwa waliotafuta elimu na fadhila. Watu hawa wakubwa wanapaswa kubaki katika kumbukumbu za jamii na dua ziendelee kufanywa kwa ajili yao.

Ayatullah Salehi, huku akisisitiza hadhi ya juu ya misingi ya kielimu ya marehemu Mirza al-Na’ini katika elimu ya usul, alisema kuwa misingi ya kiusuli ya fakihi huyu mkubwa ilikuwa na nafasi ya juu sana. Aliongeza kuwa; marehemu Ayatullah al-Khu'i alikuwa akisema mara kwa mara: Sisi tulikuwa wanafunzi wa darsa zake, na yale yote tuliyofundishwa yalitokana na misingi na kanuni za Mirza al-Na’ini.

Mwisho wa mazungumzo yake, huku akieleza kuwa Mirza al-Na’ini alihesabiwa kuwa mwalimu wa kwanza katika elimu ya usul, alisema kuwa; marehemu Ayatullah al-Khu'i pia, katika kufundisha masuala ya usul, kwa kiasi kikubwa alitegemea misingi na masomo ya mwalimu wake, marehemu Mirza al-Na’ini.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha